Mwanamitandao maarufu Chief Godlove amejitokeza kukemea madai yanayoenezwa mtandaoni yakidai kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na msanii wake mchanga, Pipi Jojo.
Katika video aliyoipakia Instagram, Chief Godlove ameonyesha kukerwa na taarifa hizo, akieleza kuwa zinamkosea heshima na msanii huyo ambaye ni mtoto wa umri wa miaka 16.
Chief Godlove amesema kuwa ukaribu wake na msanii huyo unatokana na majukumu yake ya kumlea kimuziki na kumsaidia kukua katika tasnia, na si kutokana na sababu za kimapenzi kama inavyodaiwa mtandaoni.
Chief Godlove pia amethibitisha kuwa siku ikifika, atatambulisha mke wake ili kuzima uvumi huo, akionyesha kuwa anahitaji kulinda faragha ya Pipi Jojo kutokana na umri wake mdogo.
Tuhuma hizi zilianza kusambaa baada ya Chief Godlove kumpeleka Pipi Jojo kwenye sherehe ya yacht iliyolenga kusherehekea mafanikio yake mapya tangu alipotambulishwa rasmi kwenye muziki.