Entertainment

Mashabiki Kenya Wamkataa Mbosso Kisa Siasa

Mashabiki Kenya Wamkataa Mbosso Kisa Siasa

Mashabiki wa muziki nchini Kenya wameonyesha msimamo mkali dhidi ya nyimbo za msanii wa Tanzania, Mbosso, wakidai msimamo wake wa kisiasa hauendani na hisia zao.

Tukio hili lilijitokeza wazi katika tuzo za Nganya jijini Nairobi, ambapo DJ aliyekuwa akicheza muziki alikumbana na upinzani baada ya kupiga wimbo Pawa na nyimbo nyingine za bongo flava.

Badala ya kusherehekea, mashabiki walipaza sauti wakitaka muziki wa Kenya pekee, wakimtaja Toxic Lyrikali kama chaguo lao. Mbosso anadaiwa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye alichaguliwa katika uchaguzi wa Tanzania uliokumbwa na utata.

Mashabiki wa Kenya wanaonekana kuunga mkono wimbi linaloendelea nchini Tanzania, ambapo baadhi ya wananchi wameanzisha kampeni ya kuwaadhibu wasanii waliotumika kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *