Msanii wa Kenya, Stivo Simple Boy, ameongeza hatua nyingine muhimu katika safari yake ya maisha baada ya kuhitimu masomo yake na kupata Diploma katika kozi ya Hospitality.
Stivo ameshiriki furaha yake kupitia mitandao ya kijamii, akipakia picha akiwa amevalia mavazi ya mahafali pamoja na ujumbe mfupi wenye uzito mkubwa unaosomeka “God wins.”
Msanii huyo ameahidi kuendelea kutumia elimu yake kujiendeleza zaidi na kuleta mabadiliko katika maisha yake pamoja na jamii inayomzunguka.
Kuhitimu huko kunakuja wakati ambapo Stivo Simple Boy ameendelea kujipambanua kama mfano wa uthabiti na kujituma, licha ya changamoto mbalimbali alizokutana nazo katika tasnia ya muziki na maisha binafsi.