Msanii wa muziki kutoka Uganda Weasel Manizo ameibua taharuki mitandaoni baada ya kutoa kauli tata kuhusu aliyekuwa rafiki wake wa karibu, Mozey Radio, aliyefariki minane iliyopita.
Katika majibizano na wafuasi wa NUP mtandaoni, Weasel alijibu shabiki aliyemshutumu kuhusika na kifo cha Radio kwa maneno makali akidai kifo hicho kilikuwa kinastahili na kwamba hana majuto.
Kauli hiyo imezua hasira miongoni mwa mashabiki na wadau wa muziki, wengi wakihisi imedhalilisha kumbukumbu ya msanii aliyetoa mchango mkubwa katika tasnia ya burudani. Wengine wameeleza wasiwasi juu ya afya ya kiakili ya Weasel, wakitoa wito kwa wasanii wenzake kumsaidia kwani huenda anapitia msongo wa mawazo.
Mozey Radio alifariki Februari mwaka 2017 baada ya kujeruhiwa vibaya katika ugomvi uliotokea kwenye klabu moja ya usiku mjini Entebbe, na kifo chake kilitikisa muziki wa Afrika Mashariki.