Makala ya mwaka huu ya Mbio za Magari za East Africa Classic Rally yalianza leo huko Diani, Kaunti ya Kwale, ambapo dereva Piers Daykin wa Kenya, na mwenzake Lloyd Destro katika gari aina ya Datsun 280Z, waliongoza kwa kasi katika sehemu ya SS3.
Johnny Gemmell wa Afrika Kusini anashikilia nafasi ya pili, akifuatiwa kwa karibu na gwiji wa mbio za magari Baldev Chager akiendesha gari aina yaa Porsche.
Jumla ya magari 60 yaliyopasi ukaguzi wa kiufundi yalianza mbio his oleo asubuhi. Kenya inawakilishwa na madereva 12 kati ya washindani 60, kutoka mataifa 75.
Mbio za mwaka huu zitapitia kaunti za Kwale, Taita Taveta, na Kajiado. Mbio hizo zilianzishwa rasmi leo huko Diani na Katibu katika wizara ya Michezo Elijah Mwangi, ambaye alikuwa ameandamana na Naibu Gavana wa Kwale Chirema Kombo, Mwenyekiti wa mbio za East Africa Safari Classic Rally Joey Ghose, na maafisa wakuu wa serikali za kitaifa na kaunti.