Others

Rapper Toxic Lyrikali Ashinda Tuzo Mbili Kwenye Unkut HipHop Awards 2025

Rapper Toxic Lyrikali Ashinda Tuzo Mbili Kwenye Unkut HipHop Awards 2025

Msanii wa hip-hop Toxic ameweka rekodi mpya baada ya kutwaa tuzo mbili kubwa katika hafla ya Unkut Hip-Hop Awards 2025, na hivyo kuthibitisha ubabe wake katika game ya rap nchini.

Toxic alishinda tuzo ya Msanii Bora wa Kiume, akiwapiku wakali kama Khaligraph Jones, Octopizzo, Breeder LW na Masterpiece, katika kipengele kilichoonekana kuwa na ushindani mkali zaidi mwaka huu.

Sanjari na ushindi huo, Toxic pia aliibuka mshindi katika kipengele cha Wimbo Bora wa Mwaka kupitia hit yake “Chinje”, ngoma iliyotamba sana mitandaoni na kwenye vituo vya radio. Wimbo huo uliwashinda vibaya washindani waliokuwa wakipewa nafasi kubwa, akiwemo Wakadinali, Nyashinski, Buruklyn Boyz, na tena Khaligraph Jones.

Mashabiki wamepongeza mafanikio yake wakisema Toxic sasa anathibitisha kuwa nguvu mpya kwenye hip-hop imefika na inazidi kuvunja rekodi. Mwenyewe, kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliwashukuru mashabiki kwa kumuamini na kuahidi mwaka wa mafanikio makubwa zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *