Toxic Lyrikali kuachia albamu mpya kabla ya onesho lake la Qatar.

Toxic Lyrikali kuachia albamu mpya kabla ya onesho lake la Qatar.

Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Kenya, Toxic Lyrikali, amedokeza mpango wa kuachia albamu mpya kabla ya kufanya onesho lake la muziki nchini Qatar mwezi Aprili. Kupitia taarifa zake, msanii huyo amesema anapanga kutoa albamu hiyo ili kuwapa mashabiki wake nyimbo mpya kabla ya kukutana nao jukwaani katika onesho lake la kimataifa. Toxic anatarajiwa kuwapa burudani mashabiki wake walioko Doha Aprili 9 katika tukio linalosubiriwa na wapenzi wa muziki wa Afrika Mashariki wanaoishi nchini humo. Licha ya hali ya taharuki inayotokana na mvutano wa kijeshi unaoendelea Mashariki ya Kati, unaohusisha mataifa kama Marekani, Israel na Iran, maandalizi ya onesho hilo yanaendelea kama ilivyopangwa. Onesho hilo linatarajiwa kuwavutia mashabiki wengi wa muziki wa Kenya na Afrika Mashariki wanaoishi Qatar, huku likiwa fursa kwa Toxic Lyrikali kuendeleza safari yake ya kuutangaza muziki wake kimataifa.

Read More
 Toxic Lyrikali Atangaza Ujio wa Show yake Qatar

Toxic Lyrikali Atangaza Ujio wa Show yake Qatar

Msanii wa rap kutoka Kenya, Toxic Lyrikali, ametangaza rasmi onesho lake la kwanza la kimataifa litakalofanyika jijini Doha, nchini Qatar tarehe 9 Aprili katika ukumbi wa Avenue X Lounge. Kupitia kurasa zake za kijamii, Toxic Lyrikali amesema kuwa onesho hilo la Doha ni hatua kubwa katika safari yake ya muziki, akiahidi kuwapa mashabiki wake wa ughaibuni burudani kali Rapa huyo, amesema kuwa licha ya changamoto na mijadala inayoendelea mtandaoni kuhusu muziki wake, ataendelea kusonga mbele na kupanua mipaka ya kazi yake kimataifa bila uwoga wowote. Hii itakuwa mara yake ya kwanza kwa Toxic Lyrikali kutumbuiza nje ya Kenya, hatua inayotafsiriwa kama kupanuka kwa wigo wa muziki wake kimataifa. Ikumbukwe tangazo hilo limekuja siku chache tu baada ya msanii huyo kugonga vichwa vya habari kufuatia bifu yake na kundi la Buruklyn Boyz ambapo kila upande umekuwa ukiachia mfululizo wa diss tracks ukionyesha kujiamini katika ubora wao wa kazi zao.

Read More
 Toxic Lyrikali Apuuza Diss track ya Pili ya Buruklyn Boyz kwa Kuita Mchongoano

Toxic Lyrikali Apuuza Diss track ya Pili ya Buruklyn Boyz kwa Kuita Mchongoano

Rapa kutoka Kenya Toxic Lyrikali ameendelea kushikilia msimamo wake wa kupuuza mashambulizi ya kimuziki kutoka kwa kundi la Buruklyn Boyz, akiwataka wasanii hao kuja na hoja mpya zenye ubunifu badala ya kurudia mashairi na mada zilizokwisha tumika. Kupitia ujumbe aliouandika mitandaoni, Toxic ameonyesha kutoridhishwa na kiwango cha ubunifu kilichoonyeshwa kwenye diss track ya Buruklyn iitwayo Genje Sana, akidai kuwa maudhui yaliyomo kwenye diss hiyo ni ya zamani na haoni kitu kipya kinachoweza kumsukuma kujibu kile alichokiita mchongoano. Msanii huyo amesemakuwa hataki kuhusishwa na masuala yasiyokuwa na tija, akieleza kuwa kwa sasa hana muda wa kujibu kile alichokiita diss track ya kijinga. Kwa mujibu wake, anajikita zaidi katika kukuza brand yake na kufanya muziki wenye malengo makubwa kuliko kuingia kwenye mijadala isiyo na manufaa. Katika diss track ya Buruklyn Boyz iitwayo Genje Sana, wamekosoa vikali diss track ya Toxic iitwayo Dumpsite, wakidai kuwa wimbo huo ni duni na haukufikia viwango vya mashairi vinavyotarajiwa kwenye hip hop. Kundi hilo limemtaka Toxic atulie ili wamfunze namna ya kuandika mashairi makali, wakisisitiza kuwa wao wamemtangulia kwenye muziki na wana uzoefu mkubwa zaidi kwenye game.

Read More
 Toxic Lyrikali Akanusha Kuhusika na Vurugu za Donholm

Toxic Lyrikali Akanusha Kuhusika na Vurugu za Donholm

Rapa wa Kenya Toxic Lyrikali amekanusha kuhusika na vurugu zilizotokea jana katika mtaa wa Donholm, Nairobi zilizodaiwa kuhusishwa na bifu lake linaloendelea na kundi la Buruklyn Boyz. Kupitia taarifa aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Toxic Lyrikali amesema kuwa haungi mkono vitendo vya vurugu wala uharibifu wa mali. Amesema kuwa ushindani kati yake na Buruklyn Boyz unapaswa kuamuliwa kupitia muziki pekee, si mapigano ya mitaani. Aidha, aamewataka mashabiki wake kuwa watulivu na kuepuka kuingizwa katika migogoro inayoweza kuleta madhara. Kwa sasa, vita ya maneno na diss track kati yake na Buruklyn Boyz inaonekana kuendelea katika majukwaa ya muziki, huku kila upande ukijaribu kuthibitisha ubora wake kisanaa.

Read More
 Rapa Toxic Lyrikali Aachia Diss Track Kujibu Mashambulizi ya Buruklyn Boyz

Rapa Toxic Lyrikali Aachia Diss Track Kujibu Mashambulizi ya Buruklyn Boyz

Rapa Toxic Lyrikali ameapa kutoyumba wala kupoteza mwelekeo wake wa kimuziki kutokana na kile alichokiita diss track bandia kutoka kwa baadhi ya marapa wa Kenya. Akijibu moja kwa moja mashambulizi kutoka kwa kundi la Buruklyn Boyz, ambao awali walitoa diss track iliyozua gumzo mitandaoni iitwayo Stima, Toxic amesema kuwa hataruhusu bifu za mitandaoni kumvuruga katika safari yake ya kujijenga kisanii. Katika baadhi ya mistari ya wimbo wake mpya uitwao Dumpsite, Toxic amedai kuwa wakati akijenga brand yake kwa juhudi na nidhamu, baadhi ya wanaomkosoa walikuwa wakifanya muziki wa kihuni mitaani bila mwelekeo maalum. Ameongeza kuwa mafanikio aliyoyafikia hayakuja kwa bahati, bali ni matokeo ya miaka ya kazi ngumu, ubunifu na uthabiti. Rapa huyo ameenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa itachukua muda mrefu kwa marapa anaowaita bandia kufikia mafanikio yake, iwapo wataendelea kuendekeza wivu badala ya kufanya kazi kwa bidii. Kwa mujibu wake, muziki ni ushindani wa vipaji na si bifu za kijinga. Hii ni mara ya kwanza kwa Toxic kujibu diss track kwa kuingia studio na kuachia ngoma rasmi, hatua inayodhihirisha jinsi alivyochukulia kwa uzito mashambulizi kutoka kwa Buruklyn Boyz.

Read More
 Toxic Lyrikali Afichua Nchi 6 Zinazoongoza Kumsikiliza Duniani

Toxic Lyrikali Afichua Nchi 6 Zinazoongoza Kumsikiliza Duniani

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Toxic Lyrikali, ameendelea kuthibitisha ukuaji na ushawishi wake kimataifa baada ya kufichua orodha ya nchi sita zinazoongoza kwa kusikiliza muziki wake. Kwa mujibu wa takwimu hizo, Kenya inaongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kama taifa linalomsikiliza zaidi, ikifuatiwa na Jamaica katika nafasi ya pili. Nafasi ya tatu inashikiliwa na Marekani, huku Trinidad and Tobago ikifuata katika nafasi ya nne. India imejipatia nafasi ya tano kwenye orodha hiyo, huku Uingereza ikifunga orodha ya nchi sita zinazoongoza kwa kuupa muziki wa Toxic Lyrikali mapenzi makubwa. Mafanikio hayo yanaonyesha jinsi muziki wa Toxic Lyrikali unavyoendelea kuvuka mipaka na kuwafikia mashabiki kutoka mataifa mbalimbali duniani, jambo linalothibitisha ukuaji wake kwenye soko la kimataifa.

Read More
 Toxic Lyrikali Amwaibisha Wakuu Music kwa Kuanika DM zake Akilizimisha Bifu

Toxic Lyrikali Amwaibisha Wakuu Music kwa Kuanika DM zake Akilizimisha Bifu

Rapa kutoka Kenya, Toxic Lyrikali, amezua gumzo kubwa mitandaoni baada ya kuanika jumbe za faragha za WhatsApp alizodai kutumiwa na Wakuu Music, akimshinikiza kuingia kwenye bifu naye kwa lengo la kuvuta umakini wa mashabiki. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Toxic ameshare screenshots za mawasiliano hayo zikimuonyesha Wakuu Music akimkabili kuhusu madai kuwa alikuwa amemdiss kwenye nyimbo zake. Hata hivyo, Toxic amekanusha madai hayo na kudai kuwa kinachoendelea ni juhudi za kulazimisha bifu ya kutengeneza headlines. Hitmaker huyo wa Back Bencher, ameonekana kushangazwa na kitendo hicho, akisema kuwa ni jambo la kushangaza kuona mtu mzima bado anamtext akilazimisha ugomvi wa kisanii ili apate kuzungumziwa na mashabiki. Kwa mujibu wa jumbe alizochapisha, Wakuu Music anaonekana kukerwa na madai kwamba amedharauliwa katika baadhi ya mistari ya ngoma za Toxic, jambo ambalo rapa huyo amekanusha na kudai kuwa hana mpango wa kuingia kwenye bifu la bandia kwa ajili ya hype.

Read More
 Toxic Lyrikali Aidharau Diss track ya Fathermoh kwa Kuita Mchongoano

Toxic Lyrikali Aidharau Diss track ya Fathermoh kwa Kuita Mchongoano

Rapa Toxic Lyrikali ameonekana kutochukulia kwa uzito diss track iliyodaiwa kumlenga kutoka kwa msanii wa Gengetone, Fathermoh, akisema kuwa kinachoendelea si chochote zaidi ya mchongoano wa kawaida kwenye muziki. Akizungumza Insta live, Toxic Lyrikali amesema hana muda wa kujibu diss track wala kuingia kwenye mabishano ya kitoto, Akisisitiza kuwa amejikita zaidi katika kazi yake na mafanikio anayopata kwa sasa. Rapa huyo ametoa wito kwa wasanii waliomtangulia kwenye tasnia kuacha wivu unaochochewa na mafanikio ya wasanii chipukizi, akisema badala ya kushambuliana mitandaoni au kwenye nyimbo, ni bora waweke nguvu kwenye kufanya kazi na kuboresha sanaa zao. Toxic Lyrikali ameongeza kuwa anathamini upendo mkubwa anaopata kutoka kwa mashabiki wake, hasa kutoka Kenya, akisema huo ndio unaompa nguvu ya kuendelea kupiga hatua bila kuathiriwa na maneno ya pembeni.

Read More
 Rapa Toxic Lyrikali Amuaibisha Tipsy Gee kwa Kuanika Video ya Kuomba Msamaha

Rapa Toxic Lyrikali Amuaibisha Tipsy Gee kwa Kuanika Video ya Kuomba Msamaha

Rapa Toxic Lyrikali ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kuanika video inayomuonyesha msanii wa gengetone Tipsy Gee akimuomba msamaha, kufuatia mzozo wa muda mrefu uliokuwa ukiendelea kati yao. Katika video hiyo inayosambaa kwa kasi, Tipsy Gee anaonekana akiwa mpole na mnyenyekevu, akizungumza kwa sauti ya chini na kumuomba radhi Toxic Lyrikali, hali ambayo imewafanya baadhi ya mashabiki kudai kuwa alijinyenyekeza kama mtoto baada ya maneno makali aliyokuwa akitoa awali. Kwa mujibu wa Toxic Lyrikali, Tipsy Gee amekuwa akimtukana na kumdhalilisha kupitia mitandao ya kijamii kwa kipindi kirefu, hali iliyozua mvutano na maneno makali baina ya wasanii hao wawili. Hata hivyo, mambo yalichukua mkondo mpya baada ya Toxic kuchapisha video hiyo, akidai ni ushahidi kuwa mpinzani wake alitambua makosa yake na kuamua kuomba msamaha.

Read More
 Toxic Lyrikali Awapa Vijana Moyo wa Kutia Bidii Baada ya Kushare Picha Yakeya Kazi ya Mjengo

Toxic Lyrikali Awapa Vijana Moyo wa Kutia Bidii Baada ya Kushare Picha Yakeya Kazi ya Mjengo

Msanii wa muziki kutoka Kenya,Toxic Lyrikali, amewagusa wengi mitandaoni baada ya kushare picha ya zamani inayomuonesha akiwa kazini akifanya kazi ya mjengo, miaka kadhaa kabla ya kupata mafanikio kwenye muziki wake. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Toxic Lyrikali ameeleza kuwa picha hiyo ni ukumbusho wa safari yake ya maisha, akisisitiza kuwa mafanikio hayaji kwa njia za mkato bali kwa juhudi, subira na kujituma bila kukata tamaa. Mashabiki wengi wamempongeza hitmaker huyo wa Back Bencher kwa unyenyekevu na ujasiri wa kuonyesha alikotoka, wakisema ni funzo tosha kwa vijana wanaodharau kazi ndogo au kukata tamaa mapema wanapokosa mafanikio ya haraka. Kwa mujibu wa mashabiki hao, simulizi ya Toxic Lyrikali inaonyesha wazi kuwa kila kazi halali ina heshima yake, na kwamba mafanikio ni matokeo ya safari ndefu yenye changamoto nyingi.

Read More
 Rapper Toxic Lyrikali Ashinda Tuzo Mbili Kwenye Unkut HipHop Awards 2025

Rapper Toxic Lyrikali Ashinda Tuzo Mbili Kwenye Unkut HipHop Awards 2025

Msanii wa hip-hop Toxic ameweka rekodi mpya baada ya kutwaa tuzo mbili kubwa katika hafla ya Unkut Hip-Hop Awards 2025, na hivyo kuthibitisha ubabe wake katika game ya rap nchini. Toxic alishinda tuzo ya Msanii Bora wa Kiume, akiwapiku wakali kama Khaligraph Jones, Octopizzo, Breeder LW na Masterpiece, katika kipengele kilichoonekana kuwa na ushindani mkali zaidi mwaka huu. Sanjari na ushindi huo, Toxic pia aliibuka mshindi katika kipengele cha Wimbo Bora wa Mwaka kupitia hit yake “Chinje”, ngoma iliyotamba sana mitandaoni na kwenye vituo vya radio. Wimbo huo uliwashinda vibaya washindani waliokuwa wakipewa nafasi kubwa, akiwemo Wakadinali, Nyashinski, Buruklyn Boyz, na tena Khaligraph Jones. Mashabiki wamepongeza mafanikio yake wakisema Toxic sasa anathibitisha kuwa nguvu mpya kwenye hip-hop imefika na inazidi kuvunja rekodi. Mwenyewe, kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliwashukuru mashabiki kwa kumuamini na kuahidi mwaka wa mafanikio makubwa zaidi.

Read More
 Mashabiki Wapagawa Baada ya Toxic Lyrikali Kuonekana na Mrembo

Mashabiki Wapagawa Baada ya Toxic Lyrikali Kuonekana na Mrembo

Msanii anayetikisa anga la muziki kwa sasa nchini Kenya, Toxic Lyrikali, ameibua gumzo kubwa mitandaoni baada ya kushiriki kipande cha video kwenye Instagram Story akionekana akiwa kwenye mahaba mazito na mrembo asiyejulikana. Katika video hiyo, Toxic na mrembo huyo wameonekana wakifurahia ukaribu wao bila kujificha, jambo ambalo limezidisha tetesi za kimapenzi. Baadhi ya mashabiki wanasema huenda huyo ndiye mpenzi wake mpya, hasa ikizingatiwa kwamba msanii huyo hana mazoea ya kuweka warembo wala kuonyesha maisha yake ya mapenzi mitandaoni. Hata hivyo, wengine wanahisi inaweza kuwa sehemu ya maandalizi ya kazi yake mpya. Inadaiwa kuwa Toxic Lyrikali anajiandaa kuachia wimbo unaoitwa Hide & Sick akimshirikisha Mjaka Wa Fine, na kwamba tukio hilo linaweza kuwa sehemu ya kuikuza kazi hiyo kabla ya kuachiwa rasmi. Kwa sasa, mashabiki wanasubiri kwa shauku kuona kama video hiyo ilikuwa ishara ya mapenzi mapya au ni mbinu ya kuibua msisimko kuelekea ujio wa kazi yake mpya. Msanii huyo bado hajatoa tamko lolote kuhusu video hiyo.

Read More