Wanariadha wa humu nchini John Korir na Joyceline Jepkosgei waliibuka washindi wa mbio za marathoni za Valencia kwa upande wa wanaume na wanawake mtawalia wakati wa mbio hizo zilizoandaliwa leo jijiniValencia,Uhispania.
John aliandikisha muda wa saa mbili na dakika mbili na sekunde 24 na kumpiku Amanal Petros wa Ujerumani na Awet Kibrab wa Norway waliomaliza katika nafasi za pili na tatu mtawalia
.Petro alimaliza mbio hizo katika muda wa saa mbili na dakika nne na sekunde tatu ilhali Awet alihitimisha mbio hizo katika muda wa saa mbili na dakika nne na sekunde 24.
Kwa upande wa akina dada Joyceline alindikisha muda bora msimuni baada ya kuhitimisha mbio hizo katika muda wa saa mbili na dakika 14 na kumaliza wa kwanza mbele ya Mkenya mwenzake Peres Jepchirchir aliyemaliza awa pili na Chloe Herbiet wa Ubelgiji aliyemaliza katika nafasi ya tatu.