Entertainment

Muziki wa Tanzania Wapata Views Bilioni 1.225 kwenye Mtandao wa Youtube Kenya

Muziki wa Tanzania Wapata Views Bilioni 1.225 kwenye Mtandao wa Youtube Kenya

Kenya imeendelea kuthibitisha nafasi yake kama soko kubwa la muziki wa Tanzania, baada ya ripoti mpya kuonyesha kuwa mwaka 2025 mashabiki nchini humo waliangalia video za wasanii 19 wa Bongo kwa jumla ya mara bilioni 1.225 kupitia YouTube. Takwimu hizi zinaonyesha ushawishi mkubwa wa muziki wa Tanzania nchini Kenya, huku wasanii wa muziki wa kidunia na wa injili, wakipata mwamko mkubwa kutoka kwa hadhira ya Wakenya.

Kwa upande wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameongoza kwa kuzoa jumla ya views milioni 143, akifuatwa kwa karibu na Harmonize aliyepata milioni 142. Mbosso ameshika nafasi ya tatu kwa views milioni 129, huku Marioo akifunga orodha ya vinara kwa milioni 128.

Wasanii wengine wa Bongo walioendelea kung’ara nchini Kenya ni pamoja na Zuchu (milioni 103), Rayvanny (milioni 90.3), Jay Melody (milioni 68.8), Jux (milioni 55), Alikiba (milioni 54.7), Nandy (milioni 28.8), Ibraah (milioni 20), Darassa (milioni 30.9), D Voice (milioni 40.4) na Lava Lava (milioni 19.7).

Sekta ya muziki wa injili pia imepokea sapoti kubwa kutoka kwa watazamaji wa Kenya. Joel Lwaga amejipatia milioni 61.9, akifuatiwa na Rose Muhando (milioni 39.4), Zabron Singers (milioni 27.9), Christina Shusho (milioni 25) na Neema Gospel (milioni 17.2).

Kwa ujumla, jumla ya wasanii 19 kutoka Tanzania wamekusanya zaidi ya views bilioni 1.225 kutoka Kenya pekee, hatua inayoonyesha kuwa nchi hiyo inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kukuza na kueneza muziki wa Tanzania barani Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *