Entertainment

Mbosso Amuajiri Mume wa Shabiki Baada ya Ombi la Kazi Instagram

Mbosso Amuajiri Mume wa Shabiki Baada ya Ombi la Kazi Instagram

Staa wa muziki wa Bongo Fleva Mbosso Khan amegusa nyoyo za mashabiki wake baada ya kuonyesha moyo wa utu na kujali kwa kumsaidia shabiki aliyemuomba msaada wa kumpatia mume wake kazi ya udereva.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Mbosso amejibu ombi hilo lililoachwa kwenye sehemu ya maoni, ambapo shabiki huyo alieleza changamoto walizokuwa wakipitia yeye na mume wake kwa miaka mingi licha ya mume wake kuwa na ujuzi na uzoefu wa kuendesha magari. Shabiki huyo alimwomba msanii huyo amuunganishe mume wake na kazi ya udereva ili kuboresha maisha ya familia yao.

Baada ya kuona ujumbe huo, Mbosso hakusita kuchukua hatua. Msanii huyo ameagiza timu yake kumtafuta shabiki huyo na kumsaidia kufanikisha ndoto ya kumuona mume wake akipata ajira ya udereva ndani ya timu yake.

Hatua hiyo imepongezwa vikali na mashabiki pamoja na wadau wa muziki, wengi wakimwelezea Mbosso kama msanii mwenye moyo wa huruma na anayejali jamii inayomzunguka. Wengine wamesema kitendo hicho kinaonyesha kuwa umaarufu unaweza kutumika kubadilisha maisha ya watu kwa njia chanya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *