Gossip

Mwijaku Aomba Msamaha kwa Mkewe

Mwijaku Aomba Msamaha kwa Mkewe

Mtangazaji na mdau wa burudani Mwijaku ameomba msamaha kwa mkewe kufuatia sintofahamu zilizozuka hivi karibuni katika ndoa yao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwijaku amesema anatambua ana mapungufu yake kama binadamu, lakini amemuomba mkewe amtazame kwa jicho la huruma na kukumbuka safari ndefu waliopitia pamoja.

Mwijaku ameeleza kuwa tangu alipoingia kwenye ndoa, amekuwa akipambana kwa juhudi zote kuhakikisha familia yao inapiga hatua kimaisha. Amesema mafanikio aliyofikia sasa hayakuja kwa urahisi, bali yalitokana na kujituma, kujinyima na kushirikiana kama wanandoa.

Hata hivyo ameongeza kuwa licha ya changamoto zinazowakumba, bado anaamini katika ndoa yao na yuko tayari kubadilika pale inapobidi ili kulinda familia yake.

Hadi sasa, mke wa Mwijaku bado hajatoa kauli rasmi kuhusu ombi hilo la msamaha, lakini wengi wanaendelea kumuombea ndoa yao ipate suluhu na kurejea kwenye amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *