Gossip

Esma Amkingia Kifua Diamond Platnumz Baada ya Madai ya Kupaka Lipstick

Esma Amkingia Kifua Diamond Platnumz Baada ya Madai ya Kupaka Lipstick

Dada yake msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz, amejitokeza hadharani na kumtetea kaka yake kufuatia madai yaliyoenea mitandaoni kuwa Diamond alikuwa amepaka lipstick.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Esma amesema watu waache ushamba na kutoa hukumu zisizo na msingi. Kwa mujibu wake, Diamond hakupaka lipstick bali alitumia lip balm, bidhaa ya kawaida ya kutunza midomo.

Esma ameongeza kuwa lip balm hiyo ni nzuri kwa mtu yeyote kwani huifanya midomo kuwa laini na yenye unyevunyevu. Amewahimiza wanaomkosoa Diamond kujaribu kutumia kutumia lip balm badala ya kumshambulia staa huyo bila sababu za msingi.

Siku ya jana, Diamond Platnumz alichapisha picha zake mpya kwenye ukurasa wake wa Instagram, jambo lililozua mjadala mkali miongoni mwa mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii. Baadhi yao walidai kuwa muonekano wa midomo yake ulionyesha wazi matumizi ya lipstick, madai ambayo yalisambaa kwa kasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *