Entertainment

Eko Dydda Atetea Gospel ya Kisasa kwa Kuwapuuza Wakosoaji

Eko Dydda Atetea Gospel ya Kisasa kwa Kuwapuuza Wakosoaji

Msanii wa muziki wa injili kutoka Kenya, Eko Dydda, amewatolea uvivu wanaoendelea kukosoa mtindo wake mpya wa muziki wa Injili, akisisitiza kuwa hatabadilisha msimamo wake wala imani yake kwa sababu ya maneno ya watu.

Kupitia ujumbe wake uliosambaa mitandaoni, Eko Dydda amewataka wanaobeza muziki wake kupeleka lawama zao kwingine, akisema wazi kuwa hafanyi muziki kuwaridhisha wanadamu bali anamtumikia Mungu.

Msanii huyo ameeleza kuwa kila kizazi kina njia yake ya kumtukuza Mungu, na kwamba muziki wake unalenga kuwafikia vijana wa kizazi cha sasa kwa lugha na sauti wanazoelewa. Amesisitiza kuwa mtindo hauondoi ujumbe, bali ni njia tu ya kuufikisha kwa hadhira pana zaidi.

Eko Dydda amekuwa akitambulika kwa kuvaa mavazi ya kisasa, kutumia meno ya grills na kuwasilisha ujumbe wake kwa vijana kupitia lugha ya mtaani ya sheng. Mtindo ambao umeibua hisia mseto miongoni mw watu wanaodai kwamba msanii huyo huenda amepoteza mwelekeo kwa kuiga mitindo ya wasanii wa kidunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *