Entertainment

Toxic Lyrikali Afunga Mwaka 2025 na Albamu Mpya ‘ROTEEN’

Toxic Lyrikali Afunga Mwaka 2025 na Albamu Mpya ‘ROTEEN’

Msanii wa rap Toxic Lyrikali amefunga mwaka 2025 kwa kishindo baada ya kufungua rasmi ukurasa mpya wa safari yake ya muziki kwa kuachia albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ROTEEN.

Albamu hiyo inajumuisha mkusanyiko wa nyimbo tisa ambazo awali zilikuwa zimetoka mmoja mmoja, sasa zikiwa zimeunganishwa kama mradi kamili. ROTEEN inabeba nyimbo “Thugnificent,” “Sick,” “Hood,” “Long Story,” “Bud Flowers,” “Euphoria,” “Chinje,” “Step Sana,” pamoja na wimbo wa kufunga albamu, “Glitters Freestyle.”

Albamu hii inaakisi upande wa msanii anayekomaa kisanaa, akitoa ladha ya mtaani iliyochanganywa na vibe ya kisasa inayowalenga mashabiki wa hip hop na rap ya kizazi kipya. Kila wimbo unabeba hisia, ujumbe na nishati tofauti, jambo linaloifanya ROTEEN kuwa mradi unaosikiliza kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Ingawa tangazo la albamu tayari limethibitishwa rasmi, mradi mzima bado haujapakiwa kwenye YouTube, hali iliyowaacha mashabiki wakingojea kwa hamu kuona lini albamu hiyo itapatikana kwenye jukwaa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *