Tech news

Instagram Yabadilisha Mkakati wa Engagement Kupitia Hashtag

Instagram Yabadilisha Mkakati wa Engagement Kupitia Hashtag

Instagram imeweka mwelekeo mpya kwa watumiaji wake kwa kuruhusu matumizi ya hashtag tano pekee kwa kila post. Hatua hii inalenga kuondoa kelele zisizo na maana na kuimarisha ubora wa maudhui yanayopandishwa kwenye mtandao huo wa kijamii.

Kwa mujibu wa mabadiliko haya, algorithm ya Instagram sasa inalenga kusoma na kutambua maudhui yenye thamani, badala ya kutegemea wingi wa hashtag. Hii inamaanisha kuwa watumiaji wanapaswa kuchagua hashtag chache, sahihi na zinazolingana moja kwa moja na maudhui wanayoshiriki.

Watumiaji wanahimizwa kutumia hashtag zinazohusiana moja kwa moja na content ili kuongeza ushawishi. Lakini pia matumizi ya hashtag kwa kampeni na events bado yameruhusiwa, na yanaendelea kuwa njia salama ya kufikia hadhira kubwa.

Kwa mtazamo wa baadaye, ufanisi wa post hautategemea tena idadi ya hashtag, bali ubora wa content yenyewe. Reach na engagement zitajengwa kupitia maudhui bora, yenye ubunifu na yanayogusa hadhira, badala ya hashtag nyingi zisizo na mwelekeo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *