Entertainment

Inama ya Zuchu Yashusha Woza ya Nadia Mukami Kwenye Trending YouTube Kenya

Inama ya Zuchu Yashusha Woza ya Nadia Mukami Kwenye Trending YouTube Kenya

Wimbo “Inama” wa msanii wa WCB Wasafi, Zuchu, umeendelea kutikisa chati za muziki Afrika Mashariki baada ya kushika namba moja na kuishusha ngoma “Woza” ya Nadia Mukami kwenye orodha ya trending ya YouTube Kenya.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa mitandao ya kijamii, lebo ya WCB Wasafi imewashukuru mashabiki wa Kenya kwa kuonyesha upendo mkubwa kwa Zuchu na kazi zake, ikisema kuwa sapoti hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya wimbo huo kwenye soko la Kenya.

Kwa mujibu wa takwimu za YouTube, Inama imeshika namba moja ikiwa na views milioni 2.1 ndani ya siku 6 tu, kasi iliyoifanya kuongoza trending nchini Kenya.

Kwa upande mwingine, Woza ya Nadia Mukami inashikilia nafasi ya pili na views milioni 1.3 ndani ya kipindi cha wiki tatu, jambo linaloonesha ushindani mkubwa wa wasanii wa kike kutoka Tanzania na Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *