Gossip

Mume wa Zari Hassan Ahusishwa na Wizi na Shambulio Kampala

Mume wa Zari Hassan Ahusishwa na Wizi na Shambulio Kampala

Mume wa mfanyabiashara na staa wa mitandao ya kijamii Zari Hassan, Shakib Chams, anadaiwa kuhusishwa na tukio la wizi na shambulio lililotokea katika baa moja jijini Kampala, Uganda.

Kwa mujibu wa msemaji wa Polisi wa Kabalagala, Shakib aliongoza kundi la wahuni waliowavamia wateja wa baa hiyo, ambapo inadaiwa waliwajeruhi vibaya na kuwaibia simu za mkononi pamoja na mali nyingine.

Polisi wameeleza kuwa uchunguzi unaendelea, huku Shakib akiripoti kituoni na kuandikisha taarifa yake kuhusiana na madai hayo. Mamlaka zinasisitiza kuwa taratibu za kisheria zinaendelea kufuatwa ili kubaini ukweli wa tukio hilo.

Wakati huo huo, duru za kuamika zinaeleza kuwa Zari Hassan anadaiwa kuikimbia Uganda kufuatia tuhuma hizo zinazomkabili mume wake, ingawa bado hajatoa kauli yoyote rasmi kuthibitisha au kukanusha madai hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *