Sports news

Arsenal Yaibuka na Ushindi wa Mabao 3-2 Dhidi ya Bournemouth

Arsenal Yaibuka na Ushindi wa Mabao 3-2 Dhidi ya Bournemouth

Klabu ya Arsenal imeendeleza mwendo wake mzuri katika Ligi Kuu ya England baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Bournemouth katika mchezo uliopigwa ugenini.

Arsenal ilianza kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kwanza kupitia Gabriel Magalhães dakika ya 18. Hata hivyo, Bournemouth walijibu mapema kwa kusawazisha kupitia Evanilson dakika ya 10, na kufanya mchezo kuwa wa ushindani mkubwa.

Kipindi cha pili kilikuwa cha kusisimua zaidi, ambapo Declan Rice alijitokeza kuwa shujaa wa Arsenal kwa kufunga mabao mawili dakika ya 54 na 71, na kuwapa wageni uongozi wa mabao 3-1.

Bournemouth walipata bao la pili kupitia Eli Junior Kroupi dakika ya 78, lakini juhudi zao hazikutosha kuizuia Arsenal kuondoka na pointi zote tatu muhimu

Katika mechi zingine zilizopigwa jana Jumamosi, Januari 03, Aston Villa waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Nottingham Forest, Brighton & Hove Albion wakashinda 2-0 dhidi ya Burnley, huku Wolverhampton Wanderers wakipiga West Ham United kwa mabao 3-0

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *