LifeStyle

Mulamwah Awaondolea Wakenya Hofu Baada ya Mtoto wake Kuugua Ghafla

Mulamwah Awaondolea Wakenya Hofu Baada ya Mtoto wake Kuugua Ghafla

Msanii wa vichekesho kutoka Kenya, Mulamwah, amewaondolea hofu mashabiki wake na Wakenya kwa ujumla baada ya kushiriki video ya mtoto wake wa kiume akiwa katika hali nzuri na mwenye tabasamu.

Hatua hiyo imekuja saa chache tu baada ya Baby Mama wake, Ruth K, kuomba msaada akisema mtoto wao alikuwa akilia mfululizo kwa takribani siku nane, licha ya kupelekwa hospitalini mara kadhaa bila madaktari kubaini chanzo cha tatizo hilo.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Mulamwah aameposti video hii ikimuonyesha mtoto huyo akiwa mtulivu na mwenye furaha, jambo lililotafsiriwa na wengi kama ishara kuwa hali ya mtoto imeimarika.

Awali baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii, walitafsiri huenda ni imani za kishirikiana zilizompelekea mtoto huyo kuugua ugonjwa ghafla, wakimtaka Ruth K kumpeleka mtoto huyo kwa baba yake Mulamwah ili aweze kufanyiwa tabiko kwa mujibu wa jamii ya Kiluhya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *