LifeStyle

Kamene Goro Aomba Radhi Kwa Kudanganya Kuhusu Kutoka Kimapenzi na Wanaume 27

Kamene Goro Aomba Radhi Kwa Kudanganya Kuhusu Kutoka Kimapenzi na Wanaume 27

Mtangazaji wa redio kutoka Kenya, Kamene Goro, ameomba radhi kwa umma baada ya kukiri kudanganya kuhusu madai ya kutoka kimapenzi na wanaume 27.

Akizungumza kwenye podcast ya Mwakideu Live, Kamene amefichua kuwa kauli hiyo haikuwa ya kweli, bali ilikuwa sehemu ya kampeni ya afya ya uzazi iliyolenga kuwasilisha ujumbe kwa vijana na jamii kwa ujumla.

Kamene amesema kuwa tamaa ya pesa na shinikizo la kampeni hiyo vilimfanya kubuni idadi hiyo kubwa ya wanaume ili kuvutia umakini wa watu na kupeleka ujumbe wa tahadhari kuhusu tabia za ngono zisizo salama.

Hata hivyo, amekiri kosa hilo na kuomba radhi kwa mashabiki wake na jamii, akisema kuwa uaminifu wake binafsi umeathirika kutokana na hatua hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *