Msanii wa Gengetone kutoka Kenya, Fathermoh, ameachia wimbo mpya wa diss unaomlenga rapa Toxic Lyrikali, akimrushia vijembe vikali kuhusu mwelekeo wa kazi yake ya muziki na madai ya kukosa mafanikio ya kimataifa.
Katika diss track hiyo, Fathermoh anahoji uwezo wa Toxic Lyrikali kuvuka mipaka ya Kenya kimuziki, akimdharau kwa kile anachodai ni ukosefu wa show za kimataifa.
Kupitia moja ya mistari ya diss track hiyo iliyozua mjadala mkubwa, Fathermoh amesikika akiuliza, “Passport imejaa? Unabamba tu watu wa mtaa,” kauli inayodokeza kuwa umaarufu wa Lyrikali unaishia mitaani tu.
Diss track hiyo imeibua mjadala mpana miongoni mwa mashabiki wa hip hop, baadhi wakisifia ujasiri na mbinu za Fathermoh katika mashairi, huku wengine wakiona ni mwanzo wa mfululizo wa majibizano makali kwenye muziki wa rap nchini Kenya.
Hadi sasa, Toxic Lyrikali bado hajajibu rasmi mashambulizi hayo, lakini mashabiki wengi wanasubiri kuona kama atachagua kujibu kwa wimbo mwingine au kwa kauli kupitia mitandao ya kijamii.