Rapa Toxic Lyrikali ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kuanika video inayomuonyesha msanii wa gengetone Tipsy Gee akimuomba msamaha, kufuatia mzozo wa muda mrefu uliokuwa ukiendelea kati yao.
Katika video hiyo inayosambaa kwa kasi, Tipsy Gee anaonekana akiwa mpole na mnyenyekevu, akizungumza kwa sauti ya chini na kumuomba radhi Toxic Lyrikali, hali ambayo imewafanya baadhi ya mashabiki kudai kuwa alijinyenyekeza kama mtoto baada ya maneno makali aliyokuwa akitoa awali.
Kwa mujibu wa Toxic Lyrikali, Tipsy Gee amekuwa akimtukana na kumdhalilisha kupitia mitandao ya kijamii kwa kipindi kirefu, hali iliyozua mvutano na maneno makali baina ya wasanii hao wawili.
Hata hivyo, mambo yalichukua mkondo mpya baada ya Toxic kuchapisha video hiyo, akidai ni ushahidi kuwa mpinzani wake alitambua makosa yake na kuamua kuomba msamaha.