Entertainment

Toxic Lyrikali Aidharau Diss track ya Fathermoh kwa Kuita Mchongoano

Toxic Lyrikali Aidharau Diss track ya Fathermoh kwa Kuita Mchongoano

Rapa Toxic Lyrikali ameonekana kutochukulia kwa uzito diss track iliyodaiwa kumlenga kutoka kwa msanii wa Gengetone, Fathermoh, akisema kuwa kinachoendelea si chochote zaidi ya mchongoano wa kawaida kwenye muziki.

Akizungumza Insta live, Toxic Lyrikali amesema hana muda wa kujibu diss track wala kuingia kwenye mabishano ya kitoto, Akisisitiza kuwa amejikita zaidi katika kazi yake na mafanikio anayopata kwa sasa.

Rapa huyo ametoa wito kwa wasanii waliomtangulia kwenye tasnia kuacha wivu unaochochewa na mafanikio ya wasanii chipukizi, akisema badala ya kushambuliana mitandaoni au kwenye nyimbo, ni bora waweke nguvu kwenye kufanya kazi na kuboresha sanaa zao.

Toxic Lyrikali ameongeza kuwa anathamini upendo mkubwa anaopata kutoka kwa mashabiki wake, hasa kutoka Kenya, akisema huo ndio unaompa nguvu ya kuendelea kupiga hatua bila kuathiriwa na maneno ya pembeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *