Entertainment

Mwijaku Amsuta Vikali Dudu Baya Kwa Kumvunjia Heshima Mkubwa Fella

Mwijaku Amsuta Vikali Dudu Baya Kwa Kumvunjia Heshima Mkubwa Fella

Mtangazaji na mdau wa burudani, Mwijaku, amemsuta vikali msanii mkongwe wa Bongo Fleva Dudu Baya kufuatia kauli yake tata kuhusu Mkubwa Fella, ambapo Dudu Baya alinukuliwa akisema kuwa ikitokea Mkubwa Fella amefariki, hawezi kwenda kumzika.

Akizungumza kuhusu sakata hilo, Mwijaku ameeleza kusikitishwa kwake na kauli hiyo, akimtaka Dudu Baya kuwa na heshima na utu bila kujali tofauti au migogoro iliyowahi kutokea kati yao. Mwijaku amesisitiza kuwa hakuna mwanadamu aliye mkamilifu chini ya jua, hivyo ni vyema watu kujifunza kusamehe na kuacha chuki hasa pale masuala ya afya na uhai yanapohusika.

Kauli ya Mwijaku imekuja muda mfupi baada ya Dudu Baya kudai kuwa kwa sasa hakuna msanii anayeweza kumsaidia Mkubwa Fella katika kipindi hiki ambacho anaumwa, akieleza kuwa aliwanyonya na kuwapoteza wasanii wengi kwenye tasnia ya muziki wa Bongofleva..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *