Mtangazaji na mdau wa burudani, Mwijaku, amefunguka kwa uchungu namna meneja wa wasanii Mkubwa Fella aliwahi kumdharau kipindi cha nyuma kiasi cha kutomsalimia.
Akizungumza kwa hisia kali, Mwijaku amesema Mkubwa Fella hakutaka kumuona karibu yake na mara nyingi alikuwa akipuuza salamu zake kama mtu asiyefaa katika jamii.
Mwijaku amesema licha ya kudharauliwa, ataendelea kumkingia kifua serikalini ili apate msaada wa matibabu. Anasema alipopata taarifa ya kuumwa kwake hakusita kutumia nafasi na ushawishi wake kuwasilisha ajenda hiyo kwa mamlaka husika, akiamini kuwa utu na ubinadamu vinapaswa kuwa mbele kuliko chuki za zamani.
Mwijaku amedai kuwa jambo linalomuuma zaidi ni kuona baadhi ya watu waliokuwa karibu sana na Mkubwa Fella, wakitajwa kumtoroka kipindi hiki kigumu anapitia matatizo ya kiafya.