LifeStyle

Chief Godlove Akerwa na Kejeli Baada ya Gari zake Kudaiwa Kupigwa Mnada

Chief Godlove Akerwa na Kejeli Baada ya Gari zake Kudaiwa Kupigwa Mnada

Bilionea maarufu mitandaoni, Chief Godlove, ameshindwa kujiuzuia baada ya kukumbwa na wimbi la kejeli kutoka kwa mashabiki kufuatia taarifa za magari yake ya kifahari kupigwa mnada kutokana na madeni.

Kupitia taarifa aliyotoa mtandaoni, Godlove amesema licha ya changamoto anazopitia kwa sasa, tayari ameishi maisha ya utajiri ambayo wengi wanaomkejeli hawajawahi kuyaonja.
Amejigamba kuwa aliwahi kuendesha magari makubwa na ya kifahari, akisisitiza kuwa uzoefu huo hauwezi kufutwa na anguko la muda.

Tajiri huyo mwenye majigambo, ameenda mbali zaidi na kujinadi kuwa yeye ndiye kijana mwenye ushawishi mkubwa zaidi barani Afrika, akisema ana ushawishi na uwezo wa kifedha unaomzidi hata staa wa kimataifa IShowSpeed.

Godlove pia amewashambulia wanaume wanaofurahia anguko lake kiuchumi, akiwataka waache uvivu na badala yake wajikite katika kuwahudumia wapenzi wao na kujitafutia maisha bora.

Katika kauli iliyozua taharuki zaidi, bilionea huyo amewatuhumu mashabiki wake kwa kuwaita maskini, huku akiahidi kuwa atakaporejea katika hali nzuri ya kifedha, yuko tayari kuwapa pesa za bure kama ishara ya kuthibitisha uwezo wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *