LifeStyle

Rose Muhando Akanusha Tetesi za Kufunga Ndoa Kenya

Rose Muhando Akanusha Tetesi za Kufunga Ndoa Kenya

Msanii wa muziki wa injili kutoka Tanzania, Rose Muhando, ameibuka na kukanusha vikali tetesi zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa amefunga ndoa nchini Kenya.

Akizungumza kufuatia kusambaa kwa clip moja mtandaoni, Rose Muhando amesema hajawahi kuolewa na mwanaume yeyote chini ya jua, akisisitiza kuwa taarifa hizo si za kweli kabisa. Msanii huyo ameeleza kuwa ameshtushwa na madai hayo, hasa baada ya mchungaji mmoja nchini Kenya kunukuliwa katika video hiyo akidai kuwa yeye ndiye aliyemuoa.

Rose Muhando amesema madai hayo hayana msingi wowote na amewataka mashabiki wake pamoja na umma kwa ujumla kupuuza taarifa hizo, akiongeza kuwa maisha yake binafsi hayajabadilika kama inavyodaiwa mitandaoni.

Msanii huyo, anayeheshimika kwa nyimbo zake za injili, amesisitiza kuwa kwa sasa anaendelea kujikita katika huduma na kazi yake ya muziki, huku akimwachia Mungu kila jambo linalohusu maisha yake binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *