Mwanamuziki kutoka Uganda, A Pass, amefichua kuwa alipata majeraha mabaya baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Januari 15.
A Pass amesema tukio hilo lilitokea karibu na kituo cha kupigia kura, takribani mita 50 kutoka eneo la kura, alipodai kuvamiwa ghafla na wanaume watatu.
Kwa mujibu wa msanii huyo, shughuli zake za uanaharakati huenda zilichangia kwa kiasi kikubwa kushambuliwa kwake.
A Pass ameonyesha masikitiko makubwa kuhusu tukio hilo, akisema ni jambo la kusikitisha kuona raia wakishambuliwa wakati wakitekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.
A Pass, ni mfuasi mkubwa wa chama cha National Unity Platform (NUP) na amekuwa mstari wa mbele kupinga dhuluma, matumizi mabaya ya madaraka na ukandamizaji wa haki za raia nchini Uganda.