Sports news

KBL Yatangaza Udhamini wa Milioni 40 kwa Mashindano ya HSBC Sevens Nairobi

KBL Yatangaza Udhamini wa Milioni 40 kwa Mashindano ya HSBC Sevens Nairobi

Kampuni ya Kenya Breweries Limited; KBL, imetangaza udhamini wa kitita cha shilingi milioni 40 kwa mashiandano yajayo ya raga ya HSBC Sevens Nairobi, huku Kenya ikijitayarisha kuandaa mashindano hayo ya kimataifa ya Dunia kwa mara ya kwanza.

Michuano hiyo itakayoandaliwa tarehe 14 na 15 mwezi ujao katika Uwanja wa Nyayo, yataifanya Kenya kuwa taifa la pili barani Afrika, baada ya Afrika Kusini, kuandaa mashindano ya Dunia ya Raga kwa wachezaji saba kila upande.

Ufadhili huo unajumuisha shilingi milioni 20 pesa taslimu kusaidia shirikisho la raga humu nchini; KRU katika maandalizi, pamoja na shilingi milioni 12 zaidi ambazo zitatumiwa katika shughuli za kuboresha shughuli za mashabiki, na shilingi milioni 8 zaidi zilizotengewa utangazaji wa mashindano hayo.

Timu za wanaume zitakazoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Kenya, Marekani, Uruguay, Ujerumani, Canada na Ubelgiji huku timu ya wanawake zikishirikisha Kenya, Brazil, China, Hispania, Afrika Kusini na Argentina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *