LifeStyle

Mrembo wa Kenya Akataa Ndoa na Kuzaa Watoto

Mrembo wa Kenya Akataa Ndoa na Kuzaa Watoto

Socialite mwenye utata nchini Kenya, Lydia Wanjiru, amefunguka na kuweka wazi msimamo wake kuhusu maisha ya ndoa na uzazi, akisema wazi kuwa amechagua kuishi maisha bila kuolewa wala kuzaa watoto.

Kupitia Instastory yake, Lydia amesema uamuzi huo ni wa hiari yake binafsi na umetokana na kutaka kuishi maisha yanayompa amani, uhuru na fursa ya kujijenga yeye mwenyewe bila shinikizo la kijamii.

Mrembo huyo, ameeleza kuwa jamii imekuwa ikiweka matarajio makubwa kwa wanawake kuhusu ndoa na uzazi, jambo ambalo kwake halina nafasi. Amesisitiza kuwa kutokuwa na ndoa au watoto hakumaanishi kushindwa maishani, bali ni chaguo halali kama lilivyo kwa wale wanaochagua kuoa au kuzaa.

Hii si mara ya kwanza kwa mrembo huyo kugonga vichwa vya habari. Mwishoni mwa mwaka jana, Lydia Wanjiru alizua gumzo mtandaoni baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio, kitendo ambacho kiliripotiwa kumwacha na madhara makubwa kiafya. Kutokana na hali hiyo, alilazimika kuomba msaada kutoka kwa Wakenya ili kugharamia matibabu na kurejea katika hali ya kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *