LifeStyle

Eric Omondi Atangaza Kutembea Kilomita 500 Kwa Ajili ya Kusaidia Jamii

Eric Omondi Atangaza Kutembea Kilomita 500 Kwa Ajili ya Kusaidia Jamii

Mchekeshaji na mwanaharakati wa kijamii nchini Kenya, Eric Omondi, ametangaza mpango wa kutembea umbali wa kilomita 500 kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga kituo cha msaada na uokoaji cha Sisi Kwa Sisi.

Safari hiyo ya hisani itafanyika kuanzia Februari 10 hadi 14, ambapo Omondi atatembea kwa miguu kutoka Nairobi hadi Mombasa kama sehemu ya kampeni ya kuhamasisha Wakenya na wadau mbalimbali kuchangia mradi huo muhimu.

Kwa mujibu wa Eric Omondi, kituo cha Sisi Kwa Sisi Help & Rescue Centre ni mradi unaolenga kusaidia makundi yenye uhitaji mkubwa. Kituo hicho kinatarajiwa kuwa na ghala la kuhifadhi misaada, ambulansi mbili kwa ajili ya huduma za dharura, kliniki ya kutoa huduma za afya, pamoja na shule ya sekondari ya bure kwa wanafunzi wanaotoka familia zisizojiweza.

Eric Omondi amesema kuwa matembezi hayo ni sadaka yake binafsi ili kuhamasisha mshikamano wa kitaifa na kusaidia jamii zinazohitaji huduma muhimu kama afya na elimu.

Ameitoa wito kwa wananchi, viongozi na sekta binafsi kuunga mkono mpango huo kwa kuchangia na kusambaza taarifa, akisisitiza kuwa umoja wa watu wote ndio ufunguo wa kufanikisha ujenzi wa kituo hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *