Entertainment

Chin Bees Asema Aliandika Nyimbo za Navy Kenzo Bila Kulipwa

Chin Bees Asema Aliandika Nyimbo za Navy Kenzo Bila Kulipwa

Msanii kutoka Tanzania, Chin Bees, amefunguka wazi kuhusu uhasama wake na kundi la muziki la Navy Kenzo, akisema hana mapenzi nao kabisa kutokana na kile alichodai kuwa alidhulumiwa kimasilahi.

Kulingana na Chin Bees, aliandika baadhi ya nyimbo za kundi hilo lakini hakuwahi kulipwa wala kutambuliwa kwa mchango wake.

Akipiga stori na Mjini FM, amesema kuwa tukio hilo lilimuumiza sana kihisia na kitaaluma, na ndilo chanzo cha chuki yake dhidi yao. Kwa mujibu wake, maumivu aliyopitia yalikuwa makubwa kiasi cha kuathiri mtazamo wake kwao hadi leo, akisisitiza kuwa haoni sababu ya kusamehe au kusuluhisha mgogoro huo.

Chin Bees pia amesema hana nia ya kutafuta maridhiano wala kuanzisha mazungumzo ya upatanisho, akidai yaliyotokea yalimuacha na majeraha makubwa ambayo bado hajayapona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *