Gwiji wa muziki wa dancehall Vybz Kartel amethibitishwa kuwa msanii kinara wa tamasha jipya la Talanta East Afrika Festival, maonesho ya kitamaduni ya kikanda yatakayofanyika kwenye miji mitatu ya Afrika Mashariki mwezi Mei 2026.
Msanii huyo kutoka Jamaica, ambaye muziki wake una mashabiki wengi nchini Kenya na ukanda mzima, ataongoza orodha ya wasanii watakaotumbuiza katika tamasha hilo litakalofanyika Kampala, Kigali na Nairobi.
Ziara hiyo ya kihistoria itaanza kwa kishindo Mei 1, 2026, jijini Kampala, Uganda, katika uwanja wa Lugogo Cricket Oval. Siku ikayofuata, Mei 2, 2026, Kartel atahamishia burudani hiyo jijini Kigali, Rwanda, ndani ya BK Arena. Kilele cha tamasha hilo kitafanyika jijini Nairobi, Kenya, Mei 8, 2026, katika viwanja vya Laureate Gardens.
Waandaaji wa Talanta East Afrika Festival wanasema lengo la tamasha hilo ni kukuza mshikamano wa kitamaduni na burudani katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwaleta pamoja wasanii wakubwa wa kimataifa na wa ndani. Ujio wa Vybz Kartel unatarajiwa kuvutia maelfu ya mashabiki na kuongeza hadhi ya tamasha hilo jipya kwenye ramani ya burudani barani Afrika.