LifeStyle

Matokeo ya DNA Yathibitisha Judith Makokha Sio Mama Mzazi wa Bahati

Matokeo ya DNA Yathibitisha Judith Makokha Sio Mama Mzazi wa Bahati

Matokeo ya kipimo cha vinasaba kati ya mwanamuziki wa Kenya Bahati na mwanamke aliyedai kuwa mama yake mzazi Judith Makokha yametolewa rasmi, yakionyesha kuwa wawili hao hawana uhusiano wa damu.

Kwa mujibu wa ripoti ya maabara, uwezekano wa Makokha kuwa mama mzazi wa Bahati ni asilimia sifuri. Ripoti hiyo inaeleza kuwa uchambuzi wa vinasaba uligundua kutokulingana kwa alama kadhaa za kijenetiki, zikiwemo loci D3S1358 na D1S1656, hali iliyowafanya wataalamu kufikia hitimisho kuwa Makokha hawezi kuwa mzazi wa kimaumbile wa msanii huyo.

Ikumbukwe Judith Makokha alijitokeza hadharani akidai kuwa ndiye aliyemzaa Bahati na kumwacha katika makao ya watoto yatima mwaka 1993. Madai hayo yalipingwa na Bahati ambaye kwa muda mrefu amekuwa akieleza kuwa mama yake mzazi, Lucia Mueni, alifariki mwaka 1992.

Kutokana na mvutano huo wa muda mrefu, pande husika zilikubaliana kufanyiwa kipimo cha DNA ili kubaini ukweli wa madai hayo. Matokeo yaliyotolewa sasa yanathibitisha kuwa hakuna uhusiano wa kimaumbile kati ya Bahati na Judith Makokha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *