
Mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang amevuliwa kitambaa cha Unahodha katika Klabu ya Arsenal.
Hii imekuja kufuatia vitendo vya utovu wa nidhamu baada ya kuchelewa kuwasili toka Ufaransa safari ambayo haikuwa rasmi.
Kocha Mikel Arteta ametangaza rasmi hilo leo kwenye mkutano na Waandishi wa habari kuelekea mchezo wa West Ham
Aubameyang ambaye ni nyota wa timu ya Taifa ya Gabon aliondolewa pia kwenye kikosi kwenye mchezo dhidi ya Southampton wikendi iliyopita.