
Nyota wa muziki nchini Arrow Boy amekanusha tuhuma za kumtekeleza Baby mama wake.
Akijibu swali la shabiki yake aliyetaka kujua kama ana mtoto kwenye kikao cha maswali na majibu kwenye mtandao wa instagram Hitmaker huyo wa usinimwage amesema hana mwanamke yeyote zaidi ya Nadia Mukami.
Ikumbukwe mwezi Agosti mwaka huu Arrow Boy alituhumiwa kumtekeleza Baby mama wake ambaye wamedumu kwenye ndoa kwa takriban miaka kumi.
Tuhuma hizo ziliibuliwa na mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii kupitia insta story ya mwanablogu mwenye utata Edgar Obare kwenye mtandao wa Instagram.