Entertainment

BEBE COOL AWACHANA WAANDAJI WA TUZO ZA MUZIKI UGANDA

BEBE COOL AWACHANA WAANDAJI WA TUZO ZA MUZIKI UGANDA

Mkongwe wa muziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amewatolea uvivu waandaji wa tuzo za muziki nchini humo kwa kuwapa wasanii tuzo ambazo hazina muhimu wowote.

Akiwa kwenye moja ya Interview Bebe Cool amesema waandaji wa tuzo nchini Uganda wamekuwa na mazoea ya kuwapa wasanii tuzo ambazo msanii hawezi uuza na akapata pesa za kujikimu kimaisha.

Bosi huyo wa Gagamel amedokeza mpango wa kuja na tuzo yake mwakani na washindi watapokezwa kati ya shillingi laki moja na laki tatu kulingana na kipengele ambacho msanii husika atakuwa ameteuliwa kushiriki.

Kauli ya Bebe Cool imekuja  siku chache mara baada ya Spice Diana kuwachana waandaji wa tuzo nchini uganda wasimteue  kwenye tuzo zao bila kumshirikisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *