
Msanii wa muziki nchini Akothee amekanusha taarifa za kifo ambazo zilianza kusambaa mitandaoni mapema wiki hii.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Akothee ameandika ujumbe kuwatoa hofu mashabiki zake kwa kusema kwamba amesikitishwa na kitendo cha kuzushiwa kifo wakati bado yupo hai.
R.I.P ? 🤔 Msilazimishia kifo kabla wakjati wangu haujafika. Sijachukua nafasi yako kwa hii dunia. 🙏 Acheni kuandika R.I.P mapema hivi . Nipo hai na Mungu ana sababu ya kuona siku nyingine. Hata nikifa leo hakuna mtu atachukua nafasi yangu…Akothee ameandika kupitia Instagram yake.
Hitmaker huyo wa “Sweet Love “amesema yeye ni mzima wa afya na hata ugonjwa ambao ulikuwa ukimsumbua kwa muda sasa ameshapona.
Ikumbukwe Akothee amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa ambao hakuwa wazi kwa muda muda sasa jambo ambalo limepelekea baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kumzushia kifo