Akothee Akataa Wahudumu wa Benki Wanawake kwa Madai ya Kukiuka Faragha
Mwanamuziki, Akothee, ameeleza wazi kutoridhishwa kwake na namna baadhi ya wahudumu wa benki nchini Kenya, hasa wanawake, wanavyomhudumia. Kupitia kurasa zake za kijamii, Akothee amesema kuwa kuanzia mwaka 2026 hataki kuhudumiwa na wahudumu wa benki wanawake. Amedai kuwa baadhi yao wamekuwa wakimuonesha kukosa weledi wanapokutana naye kazini. Amesema kuwa mara nyingi anapoingia benki, baadhi ya wahudumu huanza kwa kumweleza jinsi wanavyomfuatilia mitandaoni na namna anavyowapa motisha, jambo ambalo halimfurahishi. Aidha, amelalamika kuhusu ukiukwaji wa faragha akidai kuwa baadhi ya wahudumu wamekuwa wakimtambulisha kwa wateja wengine kama msanii maarufu. Kwa mujibu wake, hali hiyo humfanya ajisikie dhaifu na kukosa usalama. Hata hivyo, amesema kuwa amekuwa akipendelea kuhudumiwa na wahudumu wa kiume, akisema changamoto kubwa aliyowahi kukumbana nayo ni kupigiwa simu nje ya saa za kazi, jambo ambalo alikomesha mara moja.
Read More