Entertainment

PICHA YA MUTHONI THE DRUMMER QUEEN YATUMIKA KAMA COVER LA NEW YORK TIMES BILLBOARD

PICHA YA MUTHONI THE DRUMMER QUEEN YATUMIKA KAMA COVER LA NEW YORK TIMES BILLBOARD

Rapa wa kike nchini Muthoni the Drummer Queen anazidi kuchana mbuga kimataifa, hii ni baada ya picha yake kutumika kama cover la bango la New York Times Billboard la Nchini Marekani.

Picha ya Muthoni the Drummer Queen imerushwa mubashara kwenye bango la Times Square baada ya kutajwa kama kama msanii wa mwezi Disemba kupitia mpango wa muziki uitwao Equal ambao unaendeshwa na mtandao wa Spotify.

Rapa huyo ambaye juzi kati aliachia album yake iitwayo “River” ameshindwa kuficha furaha yake ambaye ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwahimiza marapa wa kike kuwa wajasiri na kuchukua nafasi zao kwenye tasnia ya muziki.

Muthoni the Drummer Queen anakuwa msanii wa pili wa kike nchini kwa picha yake kutumika kama cover ya bango hiyo kubwa nchini Marekani baada ya Sylivia Ssaru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *