
Msanii wa Bongofleva Country Boy ameachana rasmi na label ya Konde Music Worldwide kufuatia taarifa kwamba mkataba wake umemalizika.
Kupitia page rasmi ya KondeGang katika mtandao wa Instagram ,imethibitisha taarifa hiyo kwa kuandika ujumbe wa kumuaga na kumtakia maisha mapya, huku wakiweka wazi kuwa mkataba wake umemalizika rasmi tarehe 8 Januari mwaka wa 2022 kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Mpaka sasa rapper huyo hajazungumza chochote kuhusu taarifa hiyo, huku kukiwa na minong’ono mingi kuhusu sababu iliyo-elekea rapper huyo kutemana na record label hiyo iliyo chini ya mwanamuziki Harmonize huku hali ikitajwa kutokua shwari kwa wasanii wengine.
Country Boy (Country Wizzy) alisainiwa Konde Music Worldwide September 11, mwaka wa 2020 na kuachia kazi kadha ikiwemo EP yake βThe Father EPβ pia hits kibao kama Baby, Say, BABA na nyingine.