
Msanii mwenye mashairi yaliyoshiba kutoka nchini Tanzania Mrisho Mpoto ameeleza kushangaa na namna wasanii wa Bongofleva wanavyokilimbilia kufanya muziki wa Amapiano kutoka Afrika Kusini.
Kwenye mahojiano na E FM Mpoto amesema kuna wasanii wakubwa nchini Tanzania wana kila kitu katika muziki wao lakini anashangaa ni kipi hasa wanakitafuta kwenye Amapiano.
“Unakuta mpaka malegendary wakubwa wameingia kwenye Amapiano wote, ukisikikiza mpaka unajiuliza hata huyu, anatafuta nini sasa kiki au anatafuta hela wakati anayo, huyu ndio angekuwa kioo, angekuwa njia”.
Inaelezwa kuwa muziki wa Amapiano ulianza mwaka 2012 huko nchini Afrika Kusini,ingawa wapo wanaodai ulianzia katika vitongoji vya Johannesburg na Soweto kisha ikasambaa kote Afrika na baadhi ya maeneo duniani.