
Mwanamuziki KRG The Don amepata pigo baada ya wimbo wake uitwao Zible aliyomshirikisha msanii wa kundi la Mbogi Genje, Guzman kuondolewa kwenye mtandao wa Youtube kwa madai ya hakimiliki.
Kulingana na ujumbe ambao KRG alishare kwenye ukurasa wake wa instagram wimbo huo ulifutwa na msanii chipukizi aitwaye Zoja K Worldwide ambaye anadai kuwa KRG alisample mdundo wake na akautumia kwenye wimbo wake , Zible na Guzman wa Mbogi Genje.
Hitmaker huyo wa “Giddem” amewakosoa washindani wake akidai kuwa wanauone muziki wake wivu huku akiwataka mashabiki zake wawe na subra wakati huu uongozi wake unaifanyia kazi suala la kurejesha wimbo wake wa zible kwenye mtandao wa youtube.
Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na krg wakidai kuwa msanii huyo huenda msanii huyo amefuta wimbo huo mwenyewe ili azungumziwe kwenye mitandao ya kijamii ikizingatiwa kuwa amekuwa akipenda kujihusisha sana na kiki.