KRG The Don Akerwa na Kauli ya Kendi Kudharau Tuzo yake

KRG The Don Akerwa na Kauli ya Kendi Kudharau Tuzo yake

Msanii wa dancehall nchini Kenya, KRG The Don, amemshambulia vikali mrembo na mtangazaji Kendi baada ya kumkosoa kufuatia ushindi wake wa tuzo ya Dancehall Artist of the Year. Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii, KRG amemtolea uvivu Kendi, akisema hana uelewa wowote kuhusu muziki wa dancehall na hana mamlaka ya kuzungumzia tasnia ya muziki. Msanii huyo amesema kuwa ushindi wake ni halali na umetokana na juhudi, kazi ngumu pamoja na mchango wake mkubwa katika kukuza dancehall nchini Kenya. Mbali na hilo, KRG amemshauri Kendi ajikite katika majukumu ya kumhudumia mume wake badala ya kuingilia masuala ya muziki, akidai muda wake kwenye tasnia tayari umepita. Kauli ya Kendi imekuja mara baada ya Kendi kudai kuwa tuzo hiyo ilipaswa kwenda kwa mkongwe wa dancehall, Redsan, akisisitiza kuwa ndiye anayestahili kutambuliwa zaidi katika tasnia kutokana na mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa dancehall nchini Kenya na kimataifa

Read More
 KRG The Don Amtupia Maneno Mazito Redsan kwa Kudharau Tuzo yake

KRG The Don Amtupia Maneno Mazito Redsan kwa Kudharau Tuzo yake

Msanii wa dancehall nchini Kenya KRG The Don amejibu mashambulizi ya maneno kutoka kwa mkongwe wa muziki wa reggae na dancehall Redsan baada ya kubezwa mtandaoni kufuatia ushindi wake katika tuzo za Kenya C Awards. Akijibu kupitia mitandao ya kijamii, KRG hakusita kumshambulia Redsan kwa maneno makali, akisema mara ya mwisho kumuona mkongwe huyo ilikuwa katika ukumbi wa mazoezi (gym) alipokuwa akifanya mazoezi kwa bidii akidaiwa kujiandaa kwa kazi ya ubaunsa. KRG hakuishia hapo, alienda mbali zaidi kwa kujitolea kumpeleka Redsan vacation ikizingatiwa kuwa kazi aliyokuwa akisaka ya ubaunsa iligonga mwamba. KRG alitangazwa kama Kenya Dancehall Artist of the Year, ushindi uliibua mjadala mkubwa mitandaoni. Baadhi ya wadau walionekana kutoridhishwa na matokeo hayo, huku Redsan akitoa kauli ya kejeli iliyotafsiriwa na wengi kama dhihaka dhidi ya ushindi huo.

Read More
 KRG The Don Atawazwa Msanii Bora wa Dancehall Kenya C Awards

KRG The Don Atawazwa Msanii Bora wa Dancehall Kenya C Awards

Msanii wa muziki wa dancehall nchini Kenya, KRG The Don, ametawazwa rasmi kama Msanii Bora wa Dancehall wa Mwaka katika tuzo za Kenya C Awards. Kupitia mitandao ya kijamii, msanii huyo ameshukuru mashabiki wake kwa kumuunga mkono na kusema ushindi huo ni uthibitisho wa juhudi, kazi ngumu na kujituma kwake katika kukuza muziki wa dancehall nchini kwao Kenya. Msanii huyo ambaye watu wamekuwa wakimchukulia poa, amesema kuwa tuzo hiyo ni ya mashabiki wake waliompa sapoti tangu mwanzo wa safari yake ya muziki. Hafla ya utoaji tuzo za Kenya C Awards huwaleta pamoja wasanii, watayarishaji na wadau mbalimbali wa tasnia ya burudani nchini Kenya kwa lengo la kutambua na kusherehekea vipaji vinavyoibuka na vile vilivyojizolea umaarufu.

Read More
 KRG The Don Aingia Kwenye Biashara ya Kutengeneza Tissue Pape

KRG The Don Aingia Kwenye Biashara ya Kutengeneza Tissue Pape

Msanii wa muziki, KRG The Don, ameonekana kupanua wigo wake wa kibiashara baada ya kuashiria kuingia katika biashara ya kuzalisha tissue paper. Kupitia Instagram Story, KRG amechapisha picha za vifurushi vya tissue paper, akizisindikiza na neno “mboka” linalomaanisha kazi. Hatua hiyo imekitafsiri kuwa msanii huyo huenda tayari ameanza rasmi shughuli za uzalishaji wa bidhaa hiyo. Ingawa KRG The Don bado hajatangaza rasmi uzinduzi wa kampuni yake, dalili zinaonyesha kuwa anaweza kuwa katika hatua za mwisho za kuanzisha biashara hiyo, huku uzinduzi rasmi ukitarajiwa kufanyika hivi karibuni. Hatua yake ya kuingia kwenye sekta ya uzalishaji wa bidhaa za matumizi ya kila siku inaonekana kama mkakati mwingine wa kuongeza vyanzo vya mapato, huku mashabiki wakingoja kwa hamu taarifa rasmi kuhusu jina la kampuni, bei na upatikanaji wa bidhaa hiyo sokoni.

Read More
 KRG The Don Aahidi Kutoa Msaada kwa Wasanii wa Bongoflev

KRG The Don Aahidi Kutoa Msaada kwa Wasanii wa Bongoflev

Msanii na mfanyabiashara wa Kenya, KRG The Don, ametangaza mpango wa kutoa msaada wa kifedha kwa baadhi ya wasanii wa Bongo wanaodaiwa kukumbwa na changamoto baada ya mashabiki kuwageuka. Kupitia chapisho lake la Instagram, KRG The Don ameweka video akionekana ndani ya gari akiwa na vibandu vya pesa vinavyokadiriwa kufikia shilingi milioni 10 za Kenya, akisema fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kuwasaidia wasanii waliopatwa na ugumu wa kimaisha. Katika ujumbe wake, KRG amesema anajiandaa kusafiri kuelekea Tanzania kwa lengo la kukutana na wasanii hao na kuwapatia msaada wa kifedha utakaowasaidia kujiendeleza, hasa katika kipindi hiki ambacho baadhi yao wanaripotiwa kukosa maonesho na kupungua kwa sapoti ya muziki wao. Hatua hiyo inakuja baada ya mashabiki wa Tanzania kususia shows na nyimbo za baadhi ya wasanii, wakidai kutoridhishwa na msimamo wao wa kisiasa, hasa kufuatia uchaguzi wa Oktoba 28 uliogubikwa na mijadala na mvutano wa kisiasa.

Read More
 KRG The Don Adokeza Kugombea Useneta Nairobi 2027 Kupitia Wimbo Mpya ‘Leo’

KRG The Don Adokeza Kugombea Useneta Nairobi 2027 Kupitia Wimbo Mpya ‘Leo’

Msanii wa muziki wa Kenya, KRG The Don, amedokeza uwezekano wa kuwania kiti cha useneta wa Kaunti ya Nairobi mwaka 2027 kupitia wimbo wake mpya uitwao “Leo.” Katika video ya wimbo huo, mashabiki wamegundua bango linalosomeka “Hon. Stephen Kiruga Kimani – Senator Nairobi County. Vote!” jambo lililotafsiriwa kama ishara ya wazi kwamba msanii huyo ana mipango ya kuingia kwenye ulingo wa siasa. Iwapo ataamua kuingia rasmi katika siasa, KRG The Don ataungana na orodha ya wasanii wa Kenya waliowahi kujaribu bahati yao kwenye uongozi wa kisiasa, akiwemo Jaguar, Bahati, na Prezzo. Ikumbukwe kuwa awali KRG The Don alishawahi kutangaza hadharani nia ya kuingia kwenye siasa, ingawa hakutaja ni wadhifa upi atakaowania wala eneo gani atalisimamia kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2027.

Read More
 KRG Afichua Madhaifu ya Mfumo wa Ulipaji Mirahaba kwa Wasanii Kenya

KRG Afichua Madhaifu ya Mfumo wa Ulipaji Mirahaba kwa Wasanii Kenya

Msanii aliyegeukia biashara kutoka Kenya, KRG the Don, amefichua madhaifu ya mfumo wa ulipaji mirahaba kwa wasanii wa Kenya baada ya kuonesha kiasi cha pesa alicholipwa kama royalty za muziki wake na Chama cha Haki za Wasanii wa Utumbuizaji Nchini Kenya (PRISK) Kupitia ukurasa wake wa Instagram stories, KRG alionesha ujumbe wa M-PESA ikibainisha kuwa alipokea KSh 3,214 pekee kama malipo ya mwaka mzima. Akiwa na kejeli, alieleza kuwa hiyo ndiyo mshahara wa mwaka mzima anayopokea kama msanii nchini Kenya, jambo lililozua mjadala mitandaoni. Kauli hiyo imeibua maswali mapya kuhusu mfumo wa ulipaji wa wasanii nchini Kenya, ambapo mashabiki na wanamuziki kadhaa wamekuwa wakilalamikia malipo duni licha ya kazi zao kuchezwa mara kwa mara kwenye redio, televisheni na majukwaa ya kidijitali. KRG, anayejulikana kwa maisha ya kifahari na uwekezaji katika biashara, alitumia kisa hicho kuonesha changamoto kubwa zinazowakabili wasanii wengi nchini katika kupata fidia stahiki kutoka kwa mashirika ya haki miliki.

Read More
 KRG The Don Apendekeza DNA ya Lazima Kama Hatua ya Kuzuia Ufisadi Kenya

KRG The Don Apendekeza DNA ya Lazima Kama Hatua ya Kuzuia Ufisadi Kenya

Mwanamuziki na mfanyabiashara KRG The Don amezua mjadala mitandaoni baada ya kupendekeza kuwa uchunguzi wa DNA wa lazima kwa kila Mkenya ndio hatua ya kwanza ya kukomesha ufisadi nchini. Kupitia ujumbe aliouchapisha mitandaoni, KRG amesema kuwa changamoto nyingi za maadili na uwajibikaji nchini zinatokana na watu kukosa uwazi kuhusu undugu na majukumu ya kifamilia. Anadai kuwa iwapo kila Mkenya atapimwa DNA, kutakuwa na uwajibikaji bora wa kifamilia na kijamii, hali ambayo itachangia kupunguza visa vya ufisadi serikalini na katika mashirika binafsi. Kulingana naye, utekelezaji wa sera hiyo unaweza kusaidia kurejesha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji katika jamii, kwani watu watakuwa na hofu ya kufichuliwa na kushinikizwa kuwajibika kwa vitendo vyao. Kauli ya KRG imepokelewa kwa mitazamo tofauti mitandaoni. Wafuasi wake wengine wamepongeza hoja hiyo wakisema ni wazo jipya lenye kuibua mjadala mpana, huku wengine wakikosoa wakidai haiwezi kuhusiana moja kwa moja na vita dhidi ya ufisadi bali ni suala la heshima na utaratibu wa kifamilia. KRG, ambaye mara nyingi huzua mijadala mikali kwa kauli na mitazamo yake, ameendelea kujitambulisha si tu kama msanii wa muziki wa kizazi kipya, bali pia kama sauti ya uchokozi wa hoja zinazolenga siasa na jamii.

Read More
 KRG The Don Atoa Wito wa Amani Kati ya Kenya na Tanzania Kufuatia Kuzuia kwa Wanaharakati

KRG The Don Atoa Wito wa Amani Kati ya Kenya na Tanzania Kufuatia Kuzuia kwa Wanaharakati

Msanii na mfanyabiashara maarufu wa Kenya, KRG The Don, ametoa maoni yake kuhusu tukio la wanaharakati wa Kenya waliokamatwa na kuzuiliwa nchini Tanzania hivi karibuni. Akiwa na mtazamo wa kipekee, KRG amesema licha ya wanaharakati hao kudai kuwa walikuwa wakitetea haki, huenda hawakuzingatia mbinu sahihi za kuwasilisha ujumbe wao, jambo ambalo lilichangia wao kujipata matatani. “Ni kweli wanaharakati wana jukumu la kutetea haki, lakini kuna njia sahihi za kufanya hivyo. Kuna uwezekano walihusishwa na ajenda ya kumtetea kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Mbowe, na pengine walilipwa ili kusukuma ajenda hiyo,” alisema KRG. Aidha, KRG alieleza kusikitishwa na mzozo unaoendelea mitandaoni kati ya Wakenya na Watanzania kuhusu suala hilo. Amesisitiza kuwa Kenya na Tanzania ni mataifa ya kindugu, na haipaswi kuwa na mivutano ya kijamii au kisiasa. “Mimi nimekuwa nikisafiri Tanzania mara nyingi, na kila wakati nimepokelewa kwa heshima na mapenzi makubwa. Sioni sababu ya sisi kuchochea chuki kupitia mitandao ya kijamii,” aliongeza. Katika hatua nyingine, KRG amedokeza kuwa anapanga kusafiri hivi karibuni kwenda Tanzania kwa lengo la kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kutafuta muhula mwingine wa uongozi. Kauli ya KRG imepokewa kwa mitazamo tofauti mitandaoni, huku baadhi wakimpongeza kwa msimamo wake wa kuhimiza mshikamano wa Afrika Mashariki, na wengine wakitaka uchunguzi huru kuhusu hali ya wanaharakati waliokamatwa.

Read More
 KRG The Don: “Mimi ni Msanii wa Rais, 2027 Niko Kwa Ballot!”

KRG The Don: “Mimi ni Msanii wa Rais, 2027 Niko Kwa Ballot!”

Msanii maarufu wa dancehall nchini Kenya, KRG The Don, amethibitisha nia yake ya kuingia kwenye siasa kwa kishindo. Kupitia kauli kali yenye ujasiri, KRG alitangaza kuwa atawania kiti cha ubunge mwaka 2027 kupitia chama cha UDA, huku akisisitiza kuwa hana hofu ya wakosoaji wake.  “Mimi ni msanii wa President, hakuna mtu anaweza niguza na 2027 niko kwa ballot for MP under UDA party, wa kukasirika akasirike!” alisema KRG kwa msisitizo. Kauli hiyo inaashiria kujitokeza kwake kama mmoja wa wasanii wanaotaka kuleta mabadiliko nje ya muziki na kuingia moja kwa moja katika ulingo wa kisiasa. KRG, anayejulikana kwa mtindo wake wa maisha ya kifahari na kauli zenye utata mitandaoni, anaonekana kuwa tayari kutumia umaarufu wake kama nguzo ya kujenga ushawishi wa kisiasa. Kwa muda, KRG amekuwa akihusishwa na viongozi wa ngazi ya juu serikalini, na kauli yake ya kujitambulisha kama “msanii wa President” inaweza kuashiria uhusiano wake wa karibu na viongozi wa chama tawala. Iwapo ataendelea kushikilia msimamo wake hadi 2027, huenda akaingia kwenye historia kama mmoja wa wasanii wa Kenya waliothubutu kuchukua hatua ya moja kwa moja katika uongozi wa taifa. Hii inaibua maswali mapya kuhusu nafasi ya wasanii katika siasa na uwezo wao wa kuleta mabadiliko kwa jamii kupitia uongozi rasmi.

Read More
 KRG The Don Akanusha Uhusiano na Freemasons, Afafanua Alama Zake za Mitandaoni

KRG The Don Akanusha Uhusiano na Freemasons, Afafanua Alama Zake za Mitandaoni

Msanii wa muziki wa dansi na mjasiriamali nchini Kenya, KRG The Don, amevunja ukimya wake kuhusu tuhuma za muda mrefu zinazomhusisha na kundi la kificho la Freemasons. Akiwa kwenye mahojiano ya hivi karibuni, KRG alikanusha vikali madai hayo na kueleza sababu halisi ya kutumia alama zinazodaiwa kuwa za Freemason kwenye picha na mitandao yake ya kijamii. KRG amesema kuwa watu wamekuwa wakitafsiri vibaya ishara anazotumia kwa sababu ya kukosa uelewa wa sanaa na mitindo ya kujieleza kupitia picha. Alisema kuwa alama hizo ni sehemu ya ubunifu wa kisanii na hazihusiani kwa vyovyote na imani au makundi ya kisiri.  “Mimi si Freemason na sijawahi kuwa. Watu wanapenda kuhusisha mafanikio ya mtu na mambo ya ajabu ajabu. Nimefanya kazi kwa bidii, sihitaji kutumia njia za mkato. Hizo ishara ni style tu, ni photography na creativity, si uchawi,” alisema KRG. Kwenye picha nyingi zake mtandaoni, KRG ameonekana akitumia ishara kama kuweka mikono kwa mtindo wa pembetatu au kufunika jicho moja, alama ambazo kwa muda mrefu zimehusishwa na Freemason au kundi la Illuminati. Lakini KRG anasema hayo ni mitindo ya upigaji picha ambayo wasanii wengi duniani hutumia ili kuvutia mashabiki. Aidha, msanii huyo alieleza kuwa kuna watu wanaotumia mitandao ya kijamii kusambaza propaganda na kueneza hofu kuhusu maisha ya watu mashuhuri bila ushahidi wowote. “Sio kila kitu unachoona Instagram ni kiashiria cha mambo ya ajabu. Watu wengi wananitazama kama mfano wa mafanikio, lakini badala ya kujifunza, wanabuni stori za kunivuruga. Wacha waendelee kuongea, mimi naendelea kusonga mbele,” aliongeza. KRG The Don ni mmoja wa wasanii waliopiga hatua kubwa katika tasnia ya muziki nchini Kenya, na pia amejizolea umaarufu kutokana na maisha ya kifahari anayoyaonyesha mitandaoni. Mafanikio haya yamekuwa chanzo cha uvumi mwingi kuhusu maisha yake ya binafsi, ikiwa ni pamoja na madai ya kujiunga na Freemasons ili kufanikisha ndoto zake. Hata hivyo, kwa mara ya kwanza, msanii huyo ameweka mambo wazi na kuwahakikishia mashabiki wake kuwa mafanikio yake yanatokana na juhudi halali, si imani au makundi ya kisiri.

Read More
 KRG The Don afunguka kustaafu muziki

KRG The Don afunguka kustaafu muziki

Msanii Krg The Don amedai kuwa hana mpango wa kustaafu muziki hivi karibuni hadi pale tasnia ya muziki nchini Kenya itazalisha takriban mabilionea 10. Kwenye mahojiano na SPM Buzz amesema wasanii wa Kenya wana uwezo mkubwa wa kuwa matajiri ila wanapaswa kutia bidii zaidi kwenye kazi zao ikiwemo kuwekeza katika suala la kutoa nyimbo zenye ubora. KRG The Don ambaye amekuwa akijinasibu kuwa billionea upande wa tasnia ya muziki nchini amesema kama rapa mkongwe kutoka Marekani Jay Z aliweza kufanikisha mchakato wa kuzalisha mabillionea kama Rihanna na Kanye West, haoni kitu kitakachomzuia kutengeneza mazingira ya wasanii wa Kenya kuingiza kipato kupitia muziki wao.

Read More