
Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Papa Cidy ametoa wito kwa mashabiki zake kuanzisha kampeini ya kuchangisha shillingi millioni 3.2 za Kenya zitakazomsaidia kufufua muziki wake.
Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni Papa Cidy amesema nyimbo zake hazijakuwa zikipigwa kwenye vituo vya redio na runinga kwa sababu hana pesa za kutosha za kusukuma kazi zake za muziki.
Hitmaker huyo”Tonsuna” ameahidi kuwa ataachia muziki mzuri iwapo mashabiki zake wataitikia wito wake huo wa kumchangishi shilllingi milllioni 3.2 huku akisema kuwa ombi hilo ni mahsusi kwa mashabiki zake ambao wanaamini uwezo wake kwenye muziki.
Ikumbukwe Papa Cidy ambaye ni fundi wa manguo amekuwa kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda kwa takriban mwaka mmoja.