Entertainment

CHRIS BROWN AKANUSHA TUHUMA ZA UBAKAJI ZILIZOIBULIWA NA MWANAMKE MMOJA HUKO MAREKANI

CHRIS BROWN AKANUSHA TUHUMA ZA UBAKAJI ZILIZOIBULIWA NA MWANAMKE MMOJA HUKO MAREKANI

Mwanamuziki maarufu kutoka nchini Marekani Chris Brown ameibuka na kukanusha Taarifa  za kumbaka mwanamke mmoja huko Miami nchini Marekani Desemba 30 mwaka 2020.

Kupitia instastory kwenye mtandao wa Instagram Breezy amepuuzilia mbali tuhuma hizo kwa kudai kuwa kila mara anapoachia kazi mpya watu hutengeneza mazingira ya kumchafulia jina.

“I hope y’all see this pattern of [cap]. Whenever I’m releasing music or projects, ‘THEY’ try to pull some real b***t”. Ameandika Chris Brown.

Kauli ya Breezy imekuja mara baada ya mwanamke ambaye hakutaka jina lake lifahamike kufungulia mashtaka ya ubakaji huku akidai fidia ya zaidi ya Bilioni 2.3 za Kenya kwani kitendo hicho kilimfanya apate matatizo ikiwemo mfadhaiko wa kihisia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *