Entertainment

SHEEBAH KARUNGI AWAPA SOMO MASHABIKI ZAKE

SHEEBAH KARUNGI AWAPA SOMO MASHABIKI ZAKE

Nyota wa muziki nchini Uganda Sheebah Karungi amewaonya mashabiki zake dhidi ya kuendeshwa na shinikizo za jamii inayowazunguka.

Kupitia mitandao yake kijamii Sheebah amewataka mashabiki zake kufanya vitu ambavyo vitawapa furaha na amani kwa ajili ya kuleta matokeo chanya kwenye jamii badala ya kuwa watumwa wakufuata mkumbo ambao jamii inataka.

Hitmaker huyo wa  “Yamba Mukama” ameenda mbali na kusema kwamba mtu anaweza kuwa mfano mwema kwenye jamii yake akitumia uhuru wake kutoa hamsa kwa watu wengine kukuza na kuwekeza kwenye shughuli zao ili kuleta mabadiliko katika jamii.

Licha ya kwamba Sheebah amekuwa akiwashauri na kutia moyo vijana wenzake watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakimkosoa  mrembo huyo wakihoji kuwa ni balozi asiye na maadili kwa vijana wachanga nchini Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *