
Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Daddy Owen ametoa wito kwa wahisani kuwasaidia watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa mguu kifundo kwa maana ya Club Foot.
Kupitia Instagram Page Daddy Owen amesema watoto wengi ambao wameathiriwa na ugonjwa wa Club Foot katika jamii wameshindwa kuafikia ndoto zao kutokana na unyanyapa.
Hitmaker huyo ngoma ya “Vanity” ametoa changomoto kwa mashirika ya kijamii na wahisani wengine kujitokeza na kuwanusuru watoto wanaosumbuka na maradhi hayo kwa kuwapa matibabu.
Daddy Owen ametoa kauli hiyo alipomtembelea mwanafunzi mmoja wa kike huko visiwa vya Rusinga ambaye alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa Club Foot lakini habari njema ni kuwa amefanyiwa upasuaji na anatembea vizuri.