
Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Jose Chameleone amekiri kuwa bifu yake na wasanii wa Goodlyfe Crew Mozey Radio na Weasel Manizo lilimsaidia kukua kimuziki.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Chameleone amesema kuwa bifu zinasaidia kukuza muziki kwani kipindi cha nyuma alipokuwa anajibu diss tracks za wasanii hao kwa kuachia ngoma alizungumziwa sana kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.
Lakini pia ugomvi wake na wasanii wa Goodlife Entertainmet uliwatengenezea wasanii hao brand yao ya muziki.
Utakumbuka mwaka wa 2005 wasanii wa Goodlyf Crew walikuwa kwenye ugomvi mkali na chameleone jambo lilowafanya kuachia nyimbo za kumshambulia chameleone wakimtaja kama shetani lakini pia msanii wa mashinani.
Hata hivyo walikuja baadae wakaweka kando tofauti zao kwa faidi ya wapenzi wa muziki mzuri nchini Uganda ambao waliingia kati na kuwataka wasanii hao waache ishu ya kuendekeza chuki na badala yake washirikiane kwenye shughuli zao za kimuziki.