Entertainment

YKEE BENDA AAPA KUTOFANYA KAZI TENA NA WASANII WA NIGERIA

YKEE BENDA AAPA KUTOFANYA KAZI TENA NA WASANII WA NIGERIA

Mwanamuziki kutoka nchini uganda Ykee Benda amefunguka changamoto za kufanya kazi na wasanii wanigeria.

Katika mahojiano na Galaxy FM Ykee benda amehapa kutofanya kazi tena na wasanii wa nigeria na ikitokea amefanya nao ngoma ya pamoja itakuwa ni wao wamemtafuta

Hitmaker huyo wa “Banange” amedai baadhi ya wasanii wa Nigeria hawana moyo wa kuwasaidia wasanii wa mataifa mengine ya Afrika kwani mara nyingi wamekuwa wakiwaachia wasanii wa uganda mzigo wa kutangaza kolabo ambazo wameshafanya nao jambo ambalo anadai sio sawa.

Bosi huyo wa lebo ya muziki ya Mpaka Records ameenda mbali Zaidi na kusema kuwa wasanii wa wanigeria wanafaidi pakubwa na kolabo za wasanii wa Uganda ikizingatiwa kuwa kolabo hizo zinawasaidia kupenya kwenye soko la muziki Afrika mashariki.

Utakumbuka kipindi cha nyuma ykee benda alifanya kazi ya pamoja na msanii wa nigeria Rikado Banks kupitia singo inayokwenda kwa jina la time table lakini singo hiyo haukupata promotion ya kutosha kutokana na rikado banks kudinda kuipromote licha ya kuwa ngoma kali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *